Je, tunachakata maelezo gani??
Mgonjwa anaposhiriki katika mpango wa Max Access Solution (MAS), tunakusanya, kuhifadhi, na kuchakata (kwa pamoja, “kuchakata”) data ya kibinafsi iliyo hapa chini:
- jina lako;
- jinsia yako;
- tarehe yako ya kuzaliwa;
- nambari ya/za mawasiliano;
- anwani yako ya barua pepe;
- anwani yako ya posta;
- hospitali na daktari anayekuhudumia;
- mapato yako au hali ya kifedha (ikiwa inatumika); na
- maelezo ya mawasiliano ya mtu anayekutunza kimatibabu nyubani (ikiwa inatumika).
(kwa pamoja, “Datayako ya kibinafsi”)
Ili tutoe usaidizi na utunzaji wa kutosha, pia tutachakata data nyeti ya kibinafsi iliyo hapa chini:
- uchunguzi ya ugonjwa wako;
- tarehe ulipofnayiwa uchunguzi;
- matibabu unayopokea;
- tarehe na matokeo vyako vya PCR. (Ikiwa inatumika)
(kwa pamoja, “Data Nyeti ya Kibinafsi”)
Je, ni kwa jinsi gani na kwa nini tunachakata data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi?
Tunakusanya Data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi moja kwa moja kutoka kwako, mtunzaji wako na/au daktari wako unapotuma ombi la kushiriki kama mgonjwa katika mojawapo ya mipango yetu ya MAS. Tunachakata Data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi kwa madhumuni yafuatayo:
- kukutambua;
- kuwasiliana nawe;
- kukupa huduma za usaidizi na utunzaji wa mgonjwa;
- Kukusambazia maelezo kuhusu ugonjwa wako au matibabu unaoipokeay ;
- kutuwezesha kutii wajibu wetu chini ya sheria au kanuni zozote;
- madhumuni mengine yoyote yanayohusu usimamizi na udhibiti wa Mipango.
(kwa pamoja, “Madhumuni”).
Tunaweza kutumia data yako kwa njia ya jumla na isiyoweza kukutambulisha kwa machapisho. Hii ni inamanisha data yoyote ambayo inaweza kukutambulisha (kama. jina lako, tarehe ya kuzaliwa, anwani) itaondolewa ili kwamba hakuna mtu atakayeweza kukuhusisha na hiyo data.
Je, tutatandaza kwa nani Data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi?
Tunaweza tandaza Data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi na:
- Huluki zilizo ndani ya The Max Foundation; na
- Shirika la utekelezaji sheria au shirika la serikali ikiwa tunahitajika kufanya hivyo kisheria.
Data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi pia zimehifadhiwa katika hifadhi data yetu iliyolindwa, inayotegemea wavuti ambayo inahifadhiwa nchini Marekani.
Hatutafichua Data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi kwa wahusika wengine wowote bila idhini yako. Pia tutalinda Data yako ya Kibinafsi na/au Data Nyeti ya Kibinafsi na kuhakikisha kwamba imehifadhiwa kwa usalama.
Je, kuna athari gani za kutokubali uchakataji wa Data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi?
Ikiwa huturuhusu kuchakata Data yako ya Kibinafsi na Data Nyeti ya Kibinafsi chini ya Notisi hii ya Data ya Kibinafsi, huenda usiweze kushiriki katika mipango ya The Max Foundation.
Haki zako za ulinzi wa data:
Chini ya sheria ya ulinzi wa data, una haki ambazo ni pamoja na:
- Haki yako ya kufahamishwa – Una haki ya kufahamishwa data yako inayokusanywa, jinsi inavyotumiwa, muda itakayohifadhiwa na ikiwa itatandazwa kwa wahusika wengine wowote.
- Haki yako ya ufikiaji – Una haki ya kuomba nakala ya maelezo yako ya kibinafsi.
- Haki yako ya kurekebisha – Una haki ya kutuomba turekebishe (sahihishe) maelezo ambayo unafikiri si sahihi au hayajakamilika.
- Haki yako ya kufuta – Una haki ya kutuuliza tufute maelezo yako ya kibinafsi katika hali fulani.
- Haki yako ya kuzuia uchakataji – Una haki ya kutuomba tuzuie uchakataji wa maelezo yako katika hali fulani.
- Haki yako ya kupinga uchakataji – Una haki ya kupinga uchakataji wa Maelezo yako ya Kibinafsi katika hali fulani.
- Haki yako ya uhamishaji wa data – Una haki ya kuomba tuhamishe maelezo uliyotupa kwa shirika lingine, au kwako, katika hali fulani.
- Haki yako ya kupata notisi ya ukiukaji – Una haki ya kuarifiwa wakati wa ukiukaji wowote wa Maelezo ya Afya Yanayolindwa ambayo hayako salama.
Hupaswi kulipa ada yoyote kwa kutumia haki zako. Ukituma ombi, tutakujibu ndani ya mwezi mmoja.
Tafadhali wasiliana nasi kwa anwani ifuatayo, ikiwa ungependa kutuma ombi:
The Max Foundation
1448 NW Market St.
Suite 500
Seattle, WA 98107
+1 (206) 778-8660
info@themaxfoundation.org